Tuesday, August 4, 2015

BOATENG AANZA MAZUNGUMZO NA SPORTING LISBON.

KIUNGO wa Schalke, Kevin-Prince Boateng anajipanga kuendelea kubakia Ulaya kufuatia kuthibitisha kuanza mazungumzo na klabu kongwe ya Ureno Sporting Lisbon. Boateng mwenye umri wa miaka 28, ameripotiwa kukataa ofa kutoka klabu kongwe ya Saudi Arabia Al-Ittihad wiki iliyopita ili kusubiri timu kutoka Ulaya ambayo itamuhitaji. Sporting Lisbon wanatajwa kuanza mazungumzo na nyota huyo wa kimataifa wa Ghana ambaye amebakisha mwaka mmoja katika mkataba wake na Schalke. Boateng ambaye pia amewahi kuichezea AC Milan anatarajiwa kuuzwa kwa kitita cha euro milioni tano.

No comments:

Post a Comment