MENEJA wa Barcelona, Luis Enrique amesema anataka Pedro abakiye ndani Camp Nou kufuatia taarifa za kuwaniwa na Manchester United. Inaripotiwa kuwa United wanajipanga kutoa kitita cha paundi milioni 22 kwa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28, lakini Enrique amesisitiza hataki kabisa mchezaji huyo kuondoka. Akihojiwa Enrique aliwaambia wanahabari kuwa Pedro ni mchezaji wa kiwango cha juu na kama kocha anataka aendelee kubakia lakini hilo litakuwa ni uamuzi wake. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa mchezaji yeyote anayetaka kuondoka ataruhusiwa lakini kwasasa hakuna taarifa kama hizo.
No comments:
Post a Comment