MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Argentina, Lionel Messi ameongeza tuzo nyingine katika orodha ndefu ya tuzo alizonazo jana baada ya kupigiwa kura kuwa mchezaji bora wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA msimu uliopita. Nyota huyo wa Barcelona alimshinda mchzaji mwenzake Luis Suarez na nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo katika tuzo hiyo ambayo ilipigiwa kura na wanahabari za michezo barani Ulaya. Msimu uliopita Messi alifanikiwa kufunga mabao 58 na kutengeneza mengine 31 hivyo kuisaidia Barcelona kushinda taji la La Liga, Kombe la Mfalme na Ligi ya Mabingwa Ulaya. Messi ndio wa kwanza kushinda tuzo hilo mara mbili baada ya kushinda pia msimu wa 2010-2011 huku hasimu wake Ronaldo akishinda tuzo hiyo msimu uliopita.
No comments:
Post a Comment