CHAMA cha Soka cha Uingereza-FA kimemlima adhabu ya kutocheza mechi tatu mshambuliaji wa Chelsea Diego Costa. Costa amelimwa adhabu hiyo kufuatia tukio lake la kumfanyia vurugu beki Laurent Koscielny katika ushindi wa mabao 2-0 waliopata dhidi ya Arsenal Jumamosi iliyopita, ingawa hata hivyo alikanusha makosa hayo. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26 alionekana katika picha za video akimuwekea mikono Koscielny usoni kwake kwa makusudi kabla ya kuzozana na Gabriel aliyepewa kadi nyekundu katika mchezo huo. Hata hivyo, FA imeifuta kadi nyekundu ya Gabriel wakidai ilitolewa kimakosa huku wakimtetea mwamuzi kwa kutoona tukio alilofanya Costa dhidi ya Koscielny. Costa sasa anatarajiwa kuukoa mchezo wa Kombe la Ligi dhidi ya Walsall baadae leo sambamba na mechi za Ligi Kuu dhidi ya Newcastle United na Southampton.
No comments:
Post a Comment