Thursday, September 3, 2015

SAMMER AMTAKA RIBERY KUWA NA SUBIRA.

MKURUGENZI wa michezo wa Bayern Munich, Matthias Sammer amemuhabalisha Franck Ribery kuwa anahitaji kuwa mvumilivu zaidi kufuatia majeruhi ya kifundo cha mguu yanayomsumbua winga huyo wa kimataifa wa Ufaransa kuchelewa kupona. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 32 hajacheza mechi yeyote toka alipoumia katika mechi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Mechi mwaka jana. Ribery mwenye ameelezea tatizo lake hilo kama janga kubwa kwani hakuna tarehe yeyote iliyotajwa ya kurejea kwake uwanjani pamoja na matibabu anayopata sasa. Nafasi ya Ribery sasa imekuwa ikishikwa na nyota a kimataifa wa Brazil Douglas Costa ambaye ameonyesha kuimudu vyema katika mechi kadhaa alizocheza. Akihojiwa Sammer amesema wote wako nyuma ya Ribery kumsaidia apone haraka lakini na yeye mwenyewe anapaswa kuwa na subira.

No comments:

Post a Comment