RAIS wa muda wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA, Issa Hayatou amesema ni jambo muhimu kwa shirikisho hilo kurejea imani kwa jumuiya. Hayatou aliwasili makao makuu ya FIFA yaliyopo jijini Zurich, Uswisi jana ikiwa ni mara ya kwanza toka alipochaguliwa kuwa kiongozi wa muda baada rais Sepp Blatter kusimamishwa. FIFA ilimsimamisha kwa siku 90 Blatter sambamba na makamu wa rais wake Michel Platini na katibu mkuu Jerome Valcke ili kupisha uchunguzi wa tuhuma za rushwa zinazowakabili. Akizungumza na wanahabari Hayatou amesema anafahamu kuwa hali sio nzuri lakini wamejipanga vyema kuhakikisha hatua za msingi ili kulijenga upya shirikisho zinafanyika. Hayatou aliendelea kudai kuwa kwasasa shirikisho hilo limejikita zaidi katika uchunguzi mkuu wa rais na kutoa ushirikiano katika uchunguzi unaoendelea.
No comments:
Post a Comment