Friday, October 9, 2015

IOC YADAI FIFA INAHITAJI RAIS KUTOKA NJE.

MGOGORO unaolikumba Shirikisho la Soka Duniani-FIFA unapaswa kuwa changamoto mpya ya kufikiria kutafuta mgombea kutoka nje mwenye uadilifu ili aweze kuja kuchukua ya Sepp Blatter aliyesimamishwa. RAIS wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki-IOC, Thomas Bach amesema FIFA lazima irejeshe uaminifu wake baada ya kufungiwa kwa Blatter, makamu wa rais Michel Platini na katibu mkuu Jerome Valcke. Shirikisho hilo linachunguza tuhuma za rushwa dhidi ya viongozi hao ambao wamekanusha kufanya kosa lolote. Bach amesema FIFA inapaswa kutambua wakati ni sasa na hawawezi kutatua tatizo kwa kufanya uchaguzi na kuteua rais mpya pekee. Bach aliendelea kudai kuwa ili FIFA iweze kurejesha heshima yake inapaswa kubadili mfumo mzima ambao kwasasa unaonekana kuwa tatizo kutokana na tuhuma zilizojitokeza.

No comments:

Post a Comment