Thursday, October 1, 2015

PELLEGRINI ADAI CITY HAWAKUSTAHILI USHINDI.

MENEJA wa Manchester City, Manuel Pellegrini amesema kikosi cha hakikustahili ushindi wa dakika za mwisho walipata katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Monchengladbach jana. Sergio Aguero aliifungia City bao la penati lililoipa ushindi wa mabao 2-1, huku Joe Hart naye akokoa penati kabla ya wapinzani wao hao hawajapata bao la kuongoza katika kipindi cha pili. Akihojiwa mara bada ya mchezo huo, Pellegrini amesema City ambao walipoteza mchezo wao kwanza dhidi ya Juventus, walikuwa na bahati kushinda mchezo huo. City wametandikwa katika mechi tatu kati ya nne walizocheza za mashindano yote, ikiwemo michezo ya Ligi Kuu dhidi ya Tottenham Hotspurs na West Ham United. Kocha huyo aliendelea kudai kuwa katika michezo dhidi ya Juventus na West Ham hawakustahili kupoteza lakini leo wameshinda ingawa haikutakiwa kuwa hivyo.

No comments:

Post a Comment