KLABU ya Barcelona imetangaza kuwa Rafinha Alcantara amekubalia kusaini mkataba mpya na timu hiyo ambao utamalizika mwaka 2020 huku akiwekewa bondi ya euro milioni 75. Rafinha amecheza mechi tatu za La Liga msimu huu akiwa na Barcelona ukiwemo mchezo dhidi ya Athletic Bilbao, Malaga na Atletico madrid. Kiungo huyo ambaye ni ndugu yake na Thiago anayekipiga Bayern Munich, yuko nje ya uwanja toka Septemba mwaka huu akijiuguza majeruhi ya goti aliyopata katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya AS Roma. Pamoja na majeruhi hayo Rafinha atasaini mkataba huo mpya na klabu hiyo ambayo imemkuza kutoka katika shule yao maarufu ya La Masia.
No comments:
Post a Comment