Tuesday, November 10, 2015

RAIS WA DFB AJIUZULU.

RAIS wa Shirikisho la Soka la Ujerumani-DFB, Wolfsgang Niersbach amejiuzulu wadhifa wake huo kufuatia uchunguzi wa kukwepa kodi unaoendelea dhidi yake kufuatia malipo yaliyofanywa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Katika taarifa yake Niersbach amesema anawajibika kisiasa kutokana na malipo hayo ya paundi milioni 4.9 yaliyofanywa FIFA lakini akakanusha kufanya kosa lolote. Kiasi cha fedha hizo kinahisiwa kutumika kuwahonga maofisa wa FIFA ili waweze kuipa kura Ujerumani kuwa wenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2016. Niersbach amesema alishiriki kikamilifu kuanzia mwanzo wa kupigania zabuni ya uenyeji wa michuano hiyo mpaka mwisho lakini kamwe hakufahamu malipo yaliyofanyika kwa nyuma yake ambayo ndio yanayochunguzwa kwasasa.

No comments:

Post a Comment