Friday, November 27, 2015

STURRIDGE AUMIA TENA.

MSHAMBULIAJI wa Liverpool, Daniel Sturridge amepata majeruhi mapya baada ya kuumia mguu akiwa mazoezini na kumfanya kuukosa mchezo wa Europa League dhidi ya Bordeaux jana. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 26, alikuwa akitarajia kurejea tena uwanjani jana baada ya kupona majeruhi ya goti ambayo yalimuweka nje toka Octoba 4 mwaka huu. Hata hivyo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uingereza alipelekwa kufanyiwa vipimo baada ya kulalamika maumivu ya mguu. Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp amesema hajui sana kuhusu hali yake lakini hadhani kama ni tatizo litakalomuweka nje kwa muda mrefu. Sturridge amecheza mechi tatu pekee msimu huu huku msimu uliopita akicheza mechi 18 kutokana na majeruhi ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimuandama.

No comments:

Post a Comment