Monday, December 7, 2015

BECKHAM AIUNGA MKONO QATAR.

MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, David Beckham anaamini michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2022 inapaswa kufanyika nchini Qatar pamoja na mkanganyiko uliojitokeza kuhusiana na jinsi walivyopata haki ya kuandaa michuano hiyo. Mamlaka za Uswisi na Marekani zinachunguza madai ya rushwa ambayo yanadaiwa kutawala katika mchakato wa kutafuta haki ya kuandaa michuano hiyo nchini Urusi mwaka 2018 na 2022. Akihojiwa na kituo kimoja cha redio, Beckham amesema haijalishi kama nchi hizo zilipata nafasi hiyo kwa rushwa au la, jambo analofahamu ni kuwa tayari zimeshachaguliwa hivyo watu wanapaswa kuunga mkono. Beckham aliendelea kudai kuwa jambo hilo linahusu kupeleka mchezo wa soka katika nchi mpya hivyo anadhani wanapaswa kuendelea na hilo kwani anajua watafanikiwa. Juni mwaka huu ofisa mmoja wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA alidai kuwa Urusi na Qatar zinaweza kupoteza haki zake za kuandaa michuano hiyo kama itagunduliwa walizipata kwa rushwa.

No comments:

Post a Comment