Wednesday, December 23, 2015

BLATTER KUTUPIWA VIRAGO VYAKE NA FIFA.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA linadaiwa kumpa taarifa rais wake aliyefungia Sepp Blatter kuwa anatakiwa kuondoka katika makazi ya rais ifikapo Februari 26 wakati mbadala wake atakapokuwa amechaguliwa. Makazi hayo ya zamani yaliyopo jijini Zurich ni moja ya vitu ambavyo Blatter mwenye umri wa miaka 79 atavipoteza baada ya kufungiwa miaka nane kujishughulisha na masuala ya soka na kamati ya maadili ya shirikisho hilo Jumatatu. Mbali na makazi hayo, Blatter pia atanyang’anywa simu ya mkononi, gari pamoja na email za kiofisi ambazo zote ni mali ya FIFA. Kwasasa Blatter ataruhusiwa kutumia vitu hivyo pamoja na kuendelea kupata mshahara wake mpaka pale mkataba wake utakapomalizika Februari 26.

No comments:

Post a Comment