Monday, December 21, 2015

BLATTER, PLATINI WAFUNGIWA MIAKA NANE.

RAIS wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA Sepp Blatter na rais wa Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA Michel Platini kwa pamoja wamefungiwa miaka nane kujishughulisha na masuala yeyote yahusuyo soka kufuatia uchunguzi wa kimaadili. Wawili hao wamekutwa na hatia kufuatia malipo yasiyo ya uaminifu ya paundi milioni 1.3 ambayo Blatter alimlipa Platini mwaka 2011. Wote wawili walikanusha kufanya jambo lolote baya na adhabu hiyo itaanza kufanya kazi mara moja.m Blatter mwenye umri wa miaka 79 amekuwa rais wa FIFA toka mwaka 1998 na tayari alishatangaza kujiuzulu mara baada ya uchaguzi utakaofanyika Februari mwakani. Platini mwenye umri wa miaka 60 alikuwa akitajwa kama kiongozi wa baadaye na alikuwa na matumaini ya kuchukua nafasi ya Blatter. Mbali na dhabu hiyo Blatter pia amelimwa faini ya paundi 33,000 huku Platini yeye akilimwa faini ya paundi 54,000.

No comments:

Post a Comment