Friday, December 4, 2015

FIFA SASA HAPAKALIKI, MAOFISA 16 WENGINE MBARONI.

WAENDESHA mashtaka nchini Marekani wametangaza mashtaka mapya dhidi ya maofisa wapatao 16 wa Shirikisho la Soka Duniani-FIFA kwa kuhusika na tuhuma za rushwa baada ya uchunguzi ndani ya shirikisho hilo. Walioshitakiwa ni pamoja na maofisa wa ngazi ya juu wa Kamati ya Utendaji wanaoongoza hivi sasa na wale waliostaafu akiwemo rais wa Chama cha Soka cha Honduras Rafael Callejas. Mwanasheria Mkuu nchini Marekani Loretta Lynch amesema katika miongo miwili maofisa hao walikula njama ya kula rushwa ndani ya shirikisho hilo kiasi cha dola milioni 200. Lynch amesema kiwango cha rushwa walichopokea ni ufisadi wa kiwango cha juu hivyo suala hilo halipaswi kabisa kufumbiwa macho. Aidha kwa upande mwingine, FIFA imeendelea kusisitiza kuwa wataendelea kushirikiana na mamlaka nchini Marekani huku wakitangaza mageuzi makubwa ndani ya shirikisho hilo.

No comments:

Post a Comment