Thursday, December 3, 2015

PISTORIUS KUHUKUMIWA TENA KWA KESI YA MAUAJI.

MWANARIADHA nyota mlemavu wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius amekutwa na hatia ya mauaji baada ya Mahakama ya Rufani ya nchi hiyo kukubali rufani iliyowasilishwa na upande wa mashitaka. Upande wa mashitaka ulitaka Pistorius ahukumiwe kwa kosa la mauaji badala ya ile hukumu ya awali ya kuua bila kukusudia aliyopewa. Pistorius alimuua mpenzi wake Reeva Steenkamp Februari mwaka 2014 baada ya kumfyatulia risasi mara nne kupitia mlango wa bafuni uliokuwa umefungwa. Kwasasa wanariadha huyo alikuwa akitumikia kifungo cha nje baada ya kukaa jela kwa mwaka mmoja kati ya mitano aliyohukumiwa. Pistorius sasa atarejea tena mahakamani kwa ajili ya uamuzi wa hukumu mpya dhidi yake.

No comments:

Post a Comment