Monday, December 7, 2015

SHABIKI WA VALENCIA AANGUA NA KUFARIKI AKISHANGILIA BAO LA KUSAWAZISHA DHIDI YA BARCELONA JUZI.

KLABU ya Valencia imethibitisha kuwa shabiki wao mmoja alifariki baada ya kuanguka akishangilia bao la kusawazisha la dakika za majeruhi dhidi ya Barcelona katika mchezo waliotoka sare ya bao 1-1 Jumamosi iliyopita. Santi Mina alifunga bao hilo katika dakika ya 86 na kuifanya timu hiyo kwenda sare dhidi ya vinara hao wa La Liga huku kocha wao mpya Gary Neville akishuhudia kutoka jukwaani. Hata hivyo, shangwe hizo zimekuja na taarifa ya kufariki kwa shabiki ambapo klabu hiyo ilithibitsiha kutuma salamu za rambirambi kwa familia yake. Katika taarifa hiyo, klabu hiyo imedai kupokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa na kuahidi kuwa pamoja na familia ya shabiki huo katika kipindi hiki kigumu.

No comments:

Post a Comment