Wednesday, December 9, 2015

VAN GAAL ADAI UNITED INAIMARIKA PAMOJA NA KUTOLEWA CHAMPIONS LEAGUE.

MENEJA wa Manchester United, Louis van Gaal amesisitiza kikosi chake kimeonyesha dalili za kuimarika msimu huu pamoja na kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. United walishindwa kufuzu hatua ya timu 16 bora baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-2 kutoka kwa Wolfsburg ya Ujerumani jana. Akihojiwa Van Gaal amesema kwasasa hawezi kujitetea kwasababu wametolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya lakini ukweli ni kuwa wako vizuri kuliko ilivyokuwa mwaka uliopita. United iko katika nafasi ya nne katika Ligi Kuu, wakiwa walimaliza katika nafasi kama hiyo katika msimu wa kwanza wa Van Gaal. United sasa imeangukia katika michuano ya Europa League.

No comments:

Post a Comment