KLABU ya Barcelona imeanza kufanya usajili kwa kishindo baada ya kumaliza adhabu yao ya kutosajili waliyopewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA. Barcelona walifungiwa kutosajili kwa miezi 14 na FIFA kufuatia kukutwa na hatia ya kuvunja sheria katika usajili wa wachezaji chini ya miaka 18 waliofanya. Lakini sasa adhabu hiyo imekwisha na Barcelona sasa wameingia tena katika usajili kwa kuwaandikisha wachezaji wapya 77 katika vikosi mbalimbali vya timu hiyo kulingana na umri. Katika orodha hiyo wapo wachezaji wenye majina makubwa walioandikishwa akiwemo Arda Turan aliyetoka Atletico Madrid na Aleix Vidal katika timu ya Sevilla. Jana zaidi ya mashabiki 10,000 walijitokeza katika uwanja wa mazoezi kuishuhudia timu yao pamoja na kuwakaribisha Turan na Vidal.
No comments:
Post a Comment