Wednesday, January 13, 2016

FIFA YAMTIMUA VALCKE.

SHIRIKISHO la Soka Duniani-FIFA limethibitisha kumtimua kazi katibu mkuu wake Jerome Valcke. Kamati ya maadili ya shirikisho hilo ilikuwa imefungua kesi dhidi ya Valcke mwenye umri wa miaka 55 ambaye pia alisimamishwa kujishughulisha na masuala yeyote ya soka kutokana na tuhuma za ufisadi na sasa wameamua kusitisha kabisa mkataba wake. Valcke ana husishwa na tuhuma za kuuuza tiketi kwa bei isiyo halali katika michuano ya Kombe la Dunia lililofanyika Brazil mwaka 2014. Pamoja na kukanusha tuhuma hizo lakini shirikisho hilo limeamua kumchukulia hatua ya kusitisha kabisa mkataba wake.

No comments:

Post a Comment