WACHEZAJI wenzake kadhaa wametoa heshima zao za mwisho kwa golikipa wa zamani wa Newcastle United na timu ya taifa ya Jamhuri ya Czech Pavel Srnicek katika mazishi yake jijini Ostrava jana. Wachezaji hao wa zamani wa Newcastle Steve Howey na Steve Harper walihudhuria mazishi hayo sambamba na wachezaji wenzake wa timu ya taifa akiwemo Ludek Miklosko na nguli wa Juventus Pavel Nedved. Srnicek alifariki Desemba 29 mwaka jana akiwa na umri wa miaka 47, siku tisa baada ya kuugua ugonjwa wa moyo. Golikipa huyo alikuwa kipenzi cha mashabiki wa Newcastle katika kipindi cha kuanzia mwaka 1991 mpaka 1998 alichoichezea timu hiyo.
No comments:
Post a Comment