MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola amekiri kuwa sababu kubwa iliyomfanya kutoongeza mkataba wake katika timu hiyo ni matamanio yake ya kutaka kufundisha katika Ligi Kuu Uingereza. Akihojiwa Guardiola amesema sababu kubwa ni kutokana na kutaka kufundisha soka Ligi Kuu ingawa bado hajaamua ni klabu gani anataka kwenda. Guardiola aliendelea kudai kuwa amefurahi na kuishukuru Bayern kwa uaminifu waliomuonyesha lakini anahitaji changamoto nyingine. Meneja huyo ambaye mkataba wake na Bayern unamalizika mwishoni mwa msimu huu alitua Allianz Arena mwaka 2013 baada ya kupumzika kwa mwaka mmoja toka atoke kuinoa Barcelona.
No comments:
Post a Comment