Wednesday, January 13, 2016

MAN UNITED YAANZA KUWANDA MBADALA WA DE GEA.

KLABU ya Manchester United inaripotiwa kuwa tayari kutumia fedha nyingi kwa ajili ya kusajili golikipa mpya ili kuleta ushindani au kuwa mbadala wa David De Gea. Vyombo vya habario nchini Italia vimedai kuwa United tayari wameonyesha nia ya kutaka kumnyakuwa golikipa wa AC Milan Gianluigi Donnarumma katika majira ya kiangazi na wanataka kutoa ofa ya paundi milioni 30. Pia imedaiwa kuwa Milan itakuwa tayari kupokea ofa hiyo ili waweze kumsajili tena Salvatore Sirigu ambaye amekuwa akikosa muda wa kucheza katika klabu ya Paris Saint-Germain. Donnarumma aliibuka katika kikosi cha kwanza cha Milan mapema msimu huu na mpaka sasa amecheza mechi 11 za Serie A.

No comments:

Post a Comment