MENEJA wa Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa Alex Sanchez ataukosa mchezo wa mzuguko wa tatu wa Kombe la FA dhidi ya Sunderland ikiwa kama tahadhari. Nyota huyo wa kimataifa wa Chile amekuwa nje ya uwanja kwa zaidi ya mwezi mmoja baada ya kupata majeruhi ya msuli katika mchezo dhidi ya Norwich City Nevemba 29 mwaka jana. Sanchez alikuwa akitegemewa kurejea uwanjani kabla ya Krismasi lakini alichelewa kupona na Wenger hayuko tayari kumuwahisha kutokana na kukabiliwa na mechi ngumu za za Ligi Kuu dhidi ya Liverpool na Stoke City wiki ijayo. Akizungumza katika mtandao wa klabu hiyo, Wenger amesema taarifa mbaya aliyonayo wiki hii ni kukosekana kwa Sanchez ambaye pamoja na kupona lakini ameamua kumpa muda zaidi kama tahadhari. Wenger aliendelea kudai kuwa kiungo Mikel Arteta atakuwepo katika kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza toka Novemba 21 wakati Tomas Rosicky naye ataanza mazoezi rasmi wiki ijayo baada ya kupona majeruhi yaliyokuwa yakimsumbua.
No comments:
Post a Comment