Monday, February 1, 2016

CHELSEA BADO MGUU NJE MGUU NDANI KWA TERRY.

KLABU ya Chelsea, imesisitiza kuwa haijafunga milango ya uwezekano wa kumuongeza mkataba mwingine nahodha wake John Terry baada ya msimu huu. Terry alibainisha baada ya mchezo ambao Chelsea walishinda mabao 5-1 dhidi ya MK Dons katika mzunguko wa tano wa Kombe la FA jana, kuwa ametaarifiwa kuwa mkataba wake wa sasa hautaongezwa. Lakini wakati Chelsea wakithibitisha kukata kumpa ofa ya mkataba mpya Terry katika kikao kilichoombwa na mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 35, bado wanadai hawajafikia uamuzi wa mwisho kuhusiana na suala lake. Taarifa ya klabu hiyo imedai kuwa Teery aliomba kukutana na viongozi wiki mbili zilizopita na kuuliza kuhusu uwezekano wa kuongeza mkataba mwingine lakini jibu alilopewa halikuwa la moja kwa moja kwani mambo yanaweza kubadilika na kuongeza mkataba mwingine. Taarifa hiyo iliendelea kudai kuwa Chelsea inatambua mchango wa Terry akiwa kama mchezaji na nahodha katika kipindi chaote ambacho amekuwa akiwatumikia ndio maana bado milango iko wazi kwake.

No comments:

Post a Comment