KLABU ya Manchester United bado iko nafasi nzuri ya kuwa klabu ya kwanza Uingereza kuingiza zaidi ya paundi milioni 500 kwa mwaka pamoja na kutopata mafanikio uwanjani. Robo ya pili ya mapato imepanda kwa asilimia 26 kwa kufikia paundi milioni 133.8 huku mapato ya matangazo nayo yakipanda kwa asilimia 42.5 na kufikia paundi milioni 66.1. Mapato ya urushaji wa matangazo yamepanda kwa asilimia 31.3 na kufikia paundi milioni 37.3 na mapato ya udhamini yamepanda na kufikia paundi milioni 1.6. Lakini klabu hiyo msimu huu imejikuta ikipoteza mapato yake ya viingilio kwa asilimia 1.6 na hilo haswa linachangiwa na matokeo ambayo wamekuwa wakipata. Akizungumza na wanahabari makamu mwenyekiti wa United Ed Woodward amesema wamekuwa wakifanya vyema kibiashara pamoja na kutopata matokeo mazuri katika kipindi cgha msimu huu.
No comments:
Post a Comment