MCHEZAJI wa zamani wa kimataifa wa Uingereza, Adam Johnson amekutwa na hatia katika kosa moja la kujihusisha katika mahusiano ya kimapenzi na msichana mwenye umri wa miaka 15. Jaji wa mahakama ya Bradford Crown alimkuta Johnson na hatia ya kumtomasa kimapenzi msichana huyo. Mchezaji huyo wa zamani wa Sunderland hivi karibuni alikiri kuwahi kuwa na mahusiano hayo ila alikanusha kushiriki naye kingono. Jaji Jonathan Rose alimuonya Johnson kuwa atakabiliwa na kifungo jela na kumwambia amuage kabisa binti yake. Katika taarifa yake msichana huyo amesema amekuwa akipitia manyanyaso mengi baada ya Johnson kudai hana hatia na alifanywa kuwa yeye muongo. Johnson mwenye umri wa miaka 28 hakuonyesha hisia zozote wakati hukumu hiyo ikitolewa na alipewa dhamana mpaka siku ya kupewa kifungo chake ambacho kinatarajiwa kuwa katika wiki mbili au tatu zijazo.
No comments:
Post a Comment