
Thursday, March 17, 2016
GUARDIOLA ADAI HAOGOPI KUPANGWA NA YEYOTE.
MENEJA wa Bayern Munich, Pep Guardiola amesema hajali timu gani atakayopangiwa nayo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuichapa Juventus. Bao la kusawazisha dakika ya 90 la Thomas Muller lilitosha kupeleka mchezo huo katika muda wa nyongeza baada ya sare ya mabao 2-2, ambapo Bayern walikuja kuongeza mengine mawili na kusonga mbele kwa jumla ya mabao 6-4. Akihojiwa Guardiola amesema kama wanataka kutinga hatua ya nusu fainali hawana jinsi bali kumfunga mpinzani yeyote watakayekutana naye. Meneja huyo alikipongeza kikosi chake kwa kuonyesha ukomavu wa hali juu katika mchezo wa jana dhidi ya Juventus. Timu zingine saba zilizotinga hatua hiyo ni pamoja na Manchester City, paris Saint-Germain, Wolfsburg, Benfica, Atletico Madrid na Real Madrid.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment