Wednesday, March 9, 2016

HODGSON HAJUI KUHUSU MUSTAKABALI WAKE UINGEREZA.

KOCHA wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amekiri kuwa angependa kuendelea kuinoa nchi hiyo hata baada ya michuano ya Euro 2016 lakini uamuzi huo utakuwa sio wa kwake kufanya. Hodgson mwenye umri wa miaka 68 alisaini mkataba wa miaka minne mwaka 2012 hivyo kumaanisha kuwa mkataba huo utamalizika baada ya michuano hiyo itakayofanyika nchini Ufaransa majira ya kiangazi. Uingereza ilimaliza wakiongoza kundi lao katika michuano ya Euro mwaka 2012 chini Hodgson lakini walienguliwa kwa matuta na Italia katika hatua ya robo fainali huku pia wakishindwa kuvuka hatua ya makundi katika michuano ya Kombe la Dunia 2014 iliyofanyika nchini Brazil. Akiulizwa kuhusu mustakabali wake, Hodson amesema kama Chama cha Soka cha Uingereza-FA kitapenda aendelee kuinoa nchi hiyo atafurahi kufanya hivyo kwasababu anakipenda kibarua hicho.

No comments:

Post a Comment