MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amewapongeza wachezaji wake kwa kubadilisha hasira zao za kupoteza mchezo wa fainali ya Kombe la Ligi kwa kuonyesha kiwango bora wakati wakiichapa Manchester City kwa mabao 3-0. Liverpool walichapwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati na City katika Uwanja wa Wembley Jumapili iliyopita lakini walifanikiwa kulipa kisasi katika mchezo wa jana kwa mabao yaliyofungwa na Adam Lallana, James Milner na Roberto Firmino. Akihojiwa Klopp amesema walizungumza kuhusu fainali na mchezo huo wa jana na lilikuwa jambo muhimu kuonyesha matokeo. Meneja huyo aliendelea kudai kuwa anashukuru kwamba wachezaji wachezaji hawakuonyesha kusononeka kama ilivyodhaniwa na badala yake walionyesha mchezo bora ambao uliwapa matokeo muhimu.
No comments:
Post a Comment