NAHODHA wa Manchester City, Vincent Kompany amesema hawapaswi kufanya makosa kama wanataka kuendelea kuwepo katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu. Kipigo cha mabao 3-0 walichopata kutoka kwa Liverpool, kiliwafanya City kilizidi kukwamisha ndoto za City kwa kuwaacha katika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi wakiwa alama 10 nyuma ya vinara Leicester City. Akihojiwa Kompany amesema hawapaswi kufanya makosa zaidi lakini hakutegemea na timu zingine kupoteza mechi zao akiwalenga mahasimu wao katika mbio za ubingwa Tottenham Hotspurs na Arsenal. Beki huyo aliendelea kudai kuwa ligi ya safari hii imekuwa tofauti na ilivyozoeleka jambo ambalo ni zuri kwakuwa hakuna na mwenye uhakika wa nafasi aliyopo sasa. City wanatarajia kupambana na vibonde wanaoshika mkia Aston Villa kesho.
No comments:
Post a Comment