Tuesday, March 15, 2016

MARQUINHOS HATIHATI KUBAKIA PSG.

BEKI wa Paris Saint-Germain-PSG, Marquinhos amesema ataangalia mustakabali wake mwishoni mwa msimu huu huku tetesi za kuondoka kuelekea Barcelona zikizidi kuvuma. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amekua akipata wakati mgumu kupata nafasi katika kikosi cha kwanza mbele ya Thiago Silva na David Silva msimu huu. Kaka wa mchezaji huyo na wakala wake wameshakutana na wawakilishi wa Barcelona kuangalia uwezekano wa uhamisho wa kwenda Camp Nou ambapo meneja Luis Enrique amemuweka kinara katika wachezaji watakaokuja kuimarisha safu yake ya ulinzi. Akihojiwa kuhusiana na tetesi hizo, Marquinhos amesema kwasasa bado yuko Paris lakini hajui huko mbele itakuwaje kwani anasubiri msimu umalizike.

No comments:

Post a Comment