MENEJA wa Leicester City, Claudio Ranieri amesema hataki kushinda taji la Ligi Kuu kwa ajili ya kisasi kufuatia kuondoka kwake kutoka Chelsea mwaka 2004. Ranieri alitimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Jose Mourinho baada ya kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Arsenal waliotwaa taji hilo na nahodha wa zamani wa Chelsea Marcel Desailly anaamini Ranieri yuko kwa ajili ya kulipa kisasi cha miaka 12 iliyopita. Desailly amesema Ranieri alikuwa anyakue taji la Ligi Kuu akiwa na Chelsea mwaka 2004 lakini alipoteza kwa Arsenal hivyo kusababisha kutimuliwa na nafasi yake kuchukuliwa na Mourinho. Hata hivyo, Ranieri ambaye kikosi chake kinaongoza ligi kwa tofauti ya alama tano amesisitiza kuwa hana mpango wa kulipa kisasi. Ranieri alimkosoa Desailly na kudai kuwa anataka kushinda taji la ligi lakini sio kwa ajili ya kulipa kisasi kwani hajawahi kuwa mtu aina hiyo maisha yake yote.
No comments:
Post a Comment