MENEJA wa Atletico Madrid, Diego Simeone ametetea uamuzi wake wa kutofanya mabadiliko katika kikosi chake kwenye mchezo wa jana wa La Liga dhidi ya Deportivo La Coruna, pamoja na kukabiliwa na mchezo muhimu mbele yao wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya PSV Eindhoven. Barcelona wao walimpumzisha Luis Suarez, Ivan Rakitic na Dani Alves katika ushindi wa mabao 6-0 waliopata dhidi ya Getafe jana lakini Simeone yeye aliamua kutumia kikosi chake imara kikiwajumuisha Antoine Griezmann, Koke na Diego Godin katika ushindi wa mabao 3-0 waliopata katika Uwanja wa Vicente Calderon. Atletico bado wamebaki nyuma ta Barcelona kwa alama nane pamoja na ushindi waliopata, bado Simeone amesisitiza hatazipa umuhimu mechi wakati akijaribu kumaliza katika nafasi tatu za juu katika mechi tisa za mwisho za La Liga zilizobakia. Akihojiwa Simeone amesema wanashindana na Real Madrid na Barcelona ambao wana vikosi bora, na mchezo wao muhimu zaidi ulikuwa dhidi ya Deportivo ndio maana hakufanya mabadiliko kwenye kikosi chake.

No comments:
Post a Comment