TIMU ya wakimbizi inatarajiwa kushindana katika mshindano ya Olimpiki yatakayofanyika jijini Rio de Janeiro kipindi cha kiangazi. Jumla ya wanariadha 43 wametambuliwa katika Timu ya Wanariadha Wakimbizi ya Olimpiki-ROA, ambao watashindana kwa kupeperusha bendera ya Olimpiki. Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki, Thomas Bach amesema lengo la kuikaribisha ROA katika mashindano ya Rio ni kutuma ujumbe wa matumaini kwa wakimbizi wote duniani. Bach aliongeza kuwa timu hiyo inapewa mahitaji yote kama zilivyo timu zingine.
No comments:
Post a Comment