SHIRIKISHO la Soka la Afrika-CAF limeitoza faini Kenya ya dola 10,000 kufuatia vurugu za mashabiki wake katika mchezo wa kufuzu michuano ya Mataifa ya Afrika 2017 dhidi ya Guinea Bissau uliofanyika jijini Nairobi mwezi uliopita. CAF pia imeonya Kenya kusingatia suala la usalama wakati wa mechi za shirikisho hilo na kuongeza kuwa kama likitokea tukio kama hilo tena Harambee Stars watalazimika kucheza mechi zao za nyumbani uwanja ukiwa mtupu. Mashabiki wa Kenya walikasirika na kuanza kuvamia uwanja kutokana na kutokubaliana maamuzi yaliyotolewa wakati wa mchezo baina ya timu hizo ambao wageni Guinea Bissau walishinda bao 1-0. Nao mabingwa wa kihistoria wa Afcon Misri wametozwa faini ya dola 5,000 kwa tabia ya mashabiki wake kutumia tochi za mionzi wakati wa mchezo wao dhidi ya Nigeria.
No comments:
Post a Comment