Friday, May 6, 2016
KLOPP AWAONYA SEVILLA.
MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp amedai kikosi chake kitatumia nafasi waliyopata wakati watakapocheza na mabingwa watetezi Sevilla katika fainali ya michuano ya Europa League itakayopigwa Mei 18 mwaka huu. Baada ya kupoteza mchezo wa mkondo wa kwanza kwa kuchapwa bao 1-0 na Villarreal, Liverpool walifanikiwa kuonyesha mchezo maridadi katika Uwanja wa Anfield jana na kufanikiwa kutinga hatua hiyo kwa jumla ya mabao 3-1. Akihojiwa Klopp amesema wakati wakicheza kama walivyocheza jana, wanahitaji kila kitu na hicho ndio watakachojaribu katika mchezo wao wa fainali. Klopp aliendelea kudai kuwa watakwenda katika mchezo huo na kujaribu kufanya kila kila kitu kwa ajili ya klabu hiyo bora. Fainali hiyo itakayofanyika katika Uwanja wa St Jacob-Park jijini Basel, Uswisi itakuwa ya kwanza kwa Liverpool Ulaya toka walipofungwa mabao 2-1 na AC Milan katika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2007. Liverpool imefanikiwa kushinda fainali nane kati ya 11 za Ulaya walizocheza, tano kati ya saba katika michuano ya Kombe la Ulaya au Ligi ya Mabingwa kama inavyojulikana hivi sasa na tatu kati ya nne katika michuano ya Kombe la UEFA au Europa League.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment