Monday, June 13, 2016

EURO 2016: BAADA YA VURUGU KUZIDI, POMBE SASA KUPIGWA MARUFUKU.

SERIKALI ya Ufaransa imeitaka miji wenyeji wa mechi za michuano ya Ulaya kukataza pombe maeneo yote karibu na viwanja pamoja na sehemu maalumu za mashabiki. Hatua hiyo inakuja kufuatia siku tatu za vurugu baina ya mashabiki na polisi jijini Marseille. Shirikisho la Soka la Ulaya-UEFA linafanya uchunguzi baada ya mashabiki wa Urusi kuonekana wakikimbia kuvamia eneo la mashabiki wa Uingereza uwanjani baada ya mchezo wao uliomalizika kwa sare Jumamosi iliyopita. UEFA imetishia kuzifungia timu zote mbili kama vurugu za mashabiki wake zitaendelea. Serikali ya Uingereza imetoa ofa ya kutuma ziada ya polisi wake kwenda kuimarisha ulinzi katika mchezo wao ujao utakaofanyika huko Lens Alhamisi hii.

No comments:

Post a Comment