Wednesday, June 15, 2016

RONALDO AWAPONDA ICELAND.

MSHAMBULIAJI nyota wa kimataifa wa Ureno, Cristiano Ronaldo amewaponda Iceland kwa kukosa malengo baada ya timu hizo mbili kwenda sare ya bao 1-1 katika michuano ya Ulaya inayoendelea nchini Ufaransa. Nyota huyo wa Real Madrid pia alikataa kushikana mikono na wachezaji wa Iceland baada ya mchezo wao makundi uliofanyika huko Saint-Etienne. Akihojiwa Ronaldo amesema alidhani Iceland wameshinda Euro kwa jinsi walivyokuwa wakishangilia mwishoni mwa mchezo huo. Nyota huyo aliendelea kudai kuwa ni jambo la kushangaza kwani wao walijitahidi kushinda mchezo huku wapinzani wakiwa hawajafanya lolote hivyo ndio anavyoona kwa mawazo yake. Iceland taifa ambalo lina idadi ya watu 330,000 ndio linashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo, likiwa taifa dogo zaidi kuwahi kushiriki michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment