KLABU ya Chelsea inadaiwa kukaribia kuwasajili nyota wawili N’Golo Kante na Kalidou Koulibaly kwa jumla ya paundi milioni 80. Kante ambaye amekuwa mmoja kati ya viungo bora wa Ligi Kuu msimu uliopita wakati Leicester City walitawadhwa mabingwa, anadaiwa kukaribia kutua Stamford Bridge kwa kitita cha paundi milioni 30 kiasi ambacho kimekubaliwa na pande zote mbili. Kufuatia kumkosa beki wa kati wa Juventus Leonardo Bonucci, Antonio Conte sasa amegeuzia nguvu zake kwa Koulibali anayayekipiga Napoli, wakati akijaribu kuimarisha safu yake ya ulinzi. Mabingwa hao wa Serie A wanadaiwa kutaka paundi milioni 50 kwa nyota huyo mwenye umri wa miaka 25, na pamoja na Everton pia kutajwa kumuwania beki huyo Chelsea wanaamini wao ndio wenye nafasi kuba ya kumnasa.
No comments:
Post a Comment