Thursday, July 14, 2016

TANZANIA YAKWEA KWA NAFASI 13 VIWANGO FIFA.

TANZANIA imekwea kwa nafasi 13 mpaka kufikia nafasi ya 123 katika viwango vya ubora vipya vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA leo. Mwezi uliopita Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 136 lakini mwezi huu imepanda na kushinda nafasi hiyo huku kwa upande wa Afrika ikishika nafasi ya 36 ikizizidi nchi za Burundi iliyopo nafasi ya 125 duniani na 38 Afrika na Sudan Kusini nafasi ya 153 kwa 47 kwa nchi ukanda wa Afrika Mashariki. Nchi inayoongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki ni Uganda waliopo nafasi ya 69 duniani na 15 Afrika wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 86 duniani na 22 Afrika na Rwanda ndio wanaoshika nafasi ya tatu wakiwa katika nafasi ya 111 duniani na 32 Afrika. Kwa upande wa Afrika orodha hiyo bado imeendelea kushikiliwa na Algeria ambao wako nafasi ya 32 duniani wakifuatiwa na Ivory Coast katika nafasi ya 35, Ghana nafasi ya 36, Senegal nafasi ya 41 na Misri ndio anakamilisha tano bora ya Afrika wakiwa nafasi ya 43. Kwa upande wa orodha za jumla, Argentina bado wameendelea kukaa kileleni wakifuatiwa na Ubelgiji katika nafasi ya pili, Colombia nafasi ya tatu, Ujerumani nafasi ya nne, mabingwa wa Copa America Chile nafasi ya tano na mabingwa wa Ulaya Ureno wao wako nafasi ya sita.

No comments:

Post a Comment