Wednesday, August 3, 2016

CONTE KUMPA "SHAVU" N'GOLO KANTE IJUMAA.

MENEJA wa Chelsea, Antonio Conte amebainisha kuwa mchezaji mpya aliyesajiliwa kiangazi hiki N’Golo Kante atacheza walau kwa dakika 30 katika mchezo wa kirafiki wa Kombe la Kimataifa dhidi ya Chelsea Ijumaa hii. Kante amesajili na Chelsea kwa kitita cha paundi milioni 32 akitokea kwa mabingwa wa Ligi Kuu Leicester City lakini alikuwa bado hajacheza mechi yoyote kwa klabu yake hiyo mpya kufuatia kupewa mapumziko baada ya michuano ya Ulaya. Akihojiwa mara baada ya mazoezi ya kikosi chake yaliyofanyika katika Uwanja wa US Bank huko Minneapolis, Marekani, Conte amesema Kante amekuja akiwa katika hali nzuri na anatarajiwa kumtumia hata kwa kipindi kifupi katika mchezo wao wa Ijumaa. Beki huyo mwenye umri wa miaka 25 ni usajili wa pili wa Chelsea kufanya baada ya kumnasa Michy Batshuayi kutoka Marseille kwa kitita cha paundi milioni 33.

No comments:

Post a Comment