Wednesday, August 3, 2016

KLOPP ADOKEZA USAJILI ZAIDI.

MENEJA wa Liverpool, Jurgen Klopp anafikiria kutumia kipindi hiki cha usajili ili kuziba mapengo ya majeruhi walioanza kujitokeza katika kikosi chake hivi sasa. Meneja huyo raia wa Ujerumani atawakosa Mamadou Sakho, Joe Gomez na Lucas Leiva mwanzoni mwa msimu wa Ligi Kuu ambapo Liverpool inakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Arsenal Agosti 14 mwaka huu. Upande wa beki wa kushoto ndio eneo ambalo Liverpool inaweza kuliimarisha zaidi katika dirisha hili la usajili kabla ya halijafungwa mwishoni mwa mwezi huu. Akihojiwa kuhusiana na suala la usajili Klopp amesema anadhani bado kuna maeneo katika kikosi chake yanahitaji kuzibwa kutokana na wachezaji kupata majeruhi na kukosa wachezaji wa kutosha kuziba nafasi hizo.

No comments:

Post a Comment