MSHAMBULIAJI nyota wa Barcelona, Lionel Messi amebainisha kuwa mtoto wake wa kiume Thiago ana mapenzi madogo sana na mchezo wa soka ambao umemfanya baba yake kuwa bora. Tuzo kadhaa alizopata Messi, mataji manane ya la Liga na manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya inaonyesha hazijatosha mpaka kufikia hatua ya kumshawishi mtoto wake huyo mwenye umri wa miaka mitatu kuupenda mchezo huo. Akihojiwa kuhusiana na hilo, Messi amesema hamnunulii mipira mingi au kumlazimisha Thiago kucheza kwasababu anaonekana hapendi sana mchezo huo. Messi kwasasa yyuko katika majukumu ya kimataifa baada ya kubadili msimamo wake wa kustaafu kuitumikia timu ya taifa.
No comments:
Post a Comment