TANZANIA imeporomoka kwa nafasi nane mpaka kufikia nafasi ya 132 katika viwango vya ubora vipya vilivyotolewa na Shirikisho la Soka Duniani-FIFA leo. Mwezi uliopita Tanzania ilikuwa katika nafasi ya 123 lakini mwezi huu imeshuka na kushika nafasi hiyo huku kwa upande wa Afrika nako ikishuka mpaka nafasi ya 42 na kuzidiwa na Burundi inayoshika nafasi ya 129 duniani na 40 Afrika. Nchi inayoongoza kwa ukanda wa Afrika Mashariki ni Uganda waliopo nafasi ya 65 duniani na 15 Afrika wakifuatiwa na Kenya waliopo nafasi ya 91 duniani na 23 Afrika na Rwanda ndio wanaoshika nafasi ya tatu wakiwa katika nafasi ya 107 duniani na 33 Afrika. Kwa upande wa Afrika orodha hiyo sasa inaongozwa na Ivory Coast waliopanda kwa nafasi mbili mpaka nafasi ya 34, wakifuatiwa na Algeria waliopo nafasi ya 35 baada ya kuporomoka kwa nafasi tatu. Wengine ni Senegal waliop nafasi ya 39, Tunisia nafasi ya 42, Ghana wapo nafasi ya 43 baada ya kushuka kwa nafasi nane huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo-DRC wakiwa nafasi ya 51 baada ya kupanda kwa nafasi tano. Kwa upande wa orodha za jumla, Argentina bado wameendelea kukaa kileleni wakifuatiwa na Ubelgiji katika nafasi ya pili, Ujerumani nafasi ya tatu, Colombia nafasi ya nne, huku mabingwa mara tano wa Kombe la Dunia Brazil nao wakirejea katika tano bora.
No comments:
Post a Comment