NAHODHA wa Chelsea, John Terry anatarajiwa kukaa nje ya uwanja kwa kipindi cha siku 10 baada ya kupata majeruhi ya mguu. Nyota huyo mwenye umri wa miaka 35, aliumia katika sare ya mabao 2-2 waliyopata dhidi ya Swansea City Jumapili hii na alionekana akiondoka katika Uwanja wa liberty akiwa na magongo. Baadae beki huyo alituma picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ikionyesha kipatiwa matibabu. Akihojiwa kuhusu hali ya Terry mara baada ya mechi hiyo, meneja wa Chelsea Antonio Conte alidai kuwa hajui ukubwa wa tatizo la beki huyo hivyo inabidi wasubiri vipimo. Na Baada ya kufanyiwa vipimo jana sasa imebainika kuwa atakaa nje kwa kipindi cha siku 10, na kumfanya kukosa mchezo muhimu wa Ligi Kuu dhidi ya Liverpool Ijumaa hii.
No comments:
Post a Comment