BEKI wa zamani wa kimataifa wa Cameroon, Rigobert Song amelazwa hospitali baada ya kuripotiwa kupatwa na maradhi ya kiharusi. Mmoja wa wanafamilia amedai kuwa nguli huyo mwenye umri wa miaka 40 alifikishwa hospitali jijini Younde akiwa hajitambui baada ya kushambuliwa na maradhi hayo. Song ameichezea mechi 137 nchi yake huku pia akiwahi kucheza katika klabu za Liverpool na West Ham United zinazoshiriki Ligi Kuu Uingereza. Nguli huyo amekuwa akifanya kazi kama kocha wa timu ya taifa ya Chad toka alipoteuliwa Octoba mwaka jana. Mchezaji mwenzake wa zamani wa Cameroon Samuel Eto’o sambamba na wachezaji wenzake wa zamani wa Liverpool Jamie Carragher, Stan Collymore na Robbie Fowler wote walituma ujumba katika mitandao yao wa kijamii ya Twitter wakimpa pole nguli huyo.
No comments:
Post a Comment