Tuesday, November 15, 2016

ATAKAYECHEZESHA MECHI YA MAN UNITED NA ARSENAL ATAJWA.

MAOFISA wa Ligi Kuu wamethibitisha kuwa mwamuzi Andre Marriner ndiye atakayechezesha mchezo kati ya Manchester United na Arsenal katika Uwanja wa Old Trafford Jumamosi hii. Marriner hajawahi kuchezesha mechi yeyote ya Arsenal msimu huu lakini amewahi kuchezesha mechi ya kwanza kwa Jose Mourinho akiwa United wakati waliposhinda dhidi ya Bournemouth katika ufunguzi wa msimu. Mourinho anatarajiwa kurejea katika benchi lake la ufundi baada ya kumaliza kutumikia adhabu ya kufungiwa mechi moja kwa kumbugudhi mwamuzi Mark Clattenburg katika mchezo ambao United walitoka sare ya bila kufungana na Burnley. Katika mchezo huo United watakuwa bila mshambuliaji wao nyota Zlatan Ibrahimovic ambaye alipokea kadi yake ya njano ya tano toka kuanza kwa msimu huu katika ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Swansea, wakati Arsenal wao watakuwa na matumaini ya Alexis Sanchez kurejea baada ya kupata majeruhi mechi za kimataifa.

No comments:

Post a Comment