Monday, December 12, 2016

CHAMPIONS LEAGUE: ARSENAL WAPANGWA NA BAYERN TENA.

KLABU ya Arsenal kwa mara nyingine itakwaana na Bayern Munich katika hatua ya 16 bora ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wakati Manchester City wao wakivaana na As Monaco ya Ufaransa. Arsenal walikutana na mabingwa hao wa Ujerumani msimu uliopita, wakishinda mabao 2-0 katika Uwanja wa Emirates lakini walijikuta wakitolewa kwa kuchapwa mabao 5-1 walipokwenda Allianz Arena. Timu hizo pia zimewahi kukutana na katika hatua hiyo msimu wa 2012-2013 na 2013-2014 mara zote Bayern walifanikiwa kuikwamisha Arsenal na safari yao. Mechi zingine za hatua hiyo mabingwa watetezi Real Madrid watavaana na Napoli, Barcelona watacheza na Paris Saint-Germain huku Leicester City wakipangiwa kucheza na Sevilla. Wengine ni Benfica watakaocheza na Borussia Dortmund, FC Porto watagaragazana na Juventus huku Bayer Leverkusen wakipepetana na Atletico Madrid. Mechi za mkondo wa kwanza za michuano hiyo zinatarajiwa kuchezwa Februari 14 na 15 huku zile za marudiano zikichezwa Februari 21 na 22.

No comments:

Post a Comment