Friday, December 9, 2016

CHAPECOENSE YAONGEZA NYOTA MBILI KATIKA NEMBO YAKE.

KLABU ya Chapecoense imeongeza nyota mbili katika nembo yao kama sehemu ya kutoa heshima kwa wale waliopoteza maisha katika ajali ya ndege mwishoni mwa mwezi uliopita. Ndege iliyokuwa imebeba kikosi cha Chapecoense, benchi la ufundi na waandishi wa habari kadhaa kwa ajili ya mchezo wao wa mkondo wa kwanza wa fainali ya Copa Sudamericana ilianguka wakati ikikaribia katika mji wa Medellin siku mbili kabla ya mchezo hio na kuua watu 71. Toka wakati Shirikisho la Soka la Amerika Kusini-CONMEBOL liliuta mchezo huo na kuwapa taji hilo Chapecoense. Rais wa muda wa klabu hiyo Ivan Tozzo alithibitisha mwishoni mwa wiki iliyopita kuwa uamuzi huo umekuja kufuatia rasmi yaliyotumwa na klabu ya Atletico Nacional ambao ndio walikuwa wapinzani wa Chapecoense.

No comments:

Post a Comment